Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI anayeshughulikia
Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila ametembelea na kukagua miradi ya ujenzi
wa barabara za Mtili–Ifwagi na Sawala-Iyegeya, mkoani Iringa ambapo ameonesha
kuridhishwa na miradi hiyo.
Barabara hizo zinazojengwa na TARURA kwa lengo la kurahisisha
usafirishaji wa mazao ya chai, misitu, mbogamboga na mazao mengine kufika
sokoni kwa wakati.
Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu
utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana huku
akitoa wito kwa wakandarasi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia
muda uliopangwa.
Wananchi nao wametoa pongezi kwa serikali kwa kuwaletea
maendeleo yanayoonekana na yanayogusa maisha yao ya kila siku.
Barabara hizo zinatarajiwa kurahisisha usafiri, kukuza biashara na kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu kama afya na elimu katika maeneo ya vijijini.
0 Maoni