Charles Hilary Nkwanga afariki dunia leo Jijini Dar

 

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary Nkwanga, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Taarifa zinasema kwamba Charles alikuwa anaumwa na alifanyiwa operesheni ndogo huko Zanzibar na akarudi nyumbani kwake Kibamba Dar es Salaam.

Hali ya Charles ilibadilika akazidiwa na wakati anakimbizwa Hospital ya Mloganzila akafariki dunia akiwa njiani.

Msiba wa Marehemu Charles Hilary Nkwanga upo nyumbani kwake Kibamba CCM, ambapo mipango ya mazishi inaendelea kufanywa.

Chapisha Maoni

0 Maoni