Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa Uchaguzi Mkuu Ujao Utafanyika kwa Amani na Utulivu.
Alhaj Dkt,
Mwinyi ameyasema hayo alipotoa Salamu baada ya Kujumuika kwa Sala ya Ijumaa
Masjid Raudha Uliopo Darajabovu, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 4 Aprili 2025.
Amefahamisha
kuwa dhamira ya Serikali anayoiongoza ni kuona Uchaguzi huo kuwa ni Kielelezo cha
kuwepo kwa Amani ya kudumu hapa Nchini na kila Mwananchi anapata fursa ya
kutekeleza haki ya Msingi ya Kikatiba ya kupiga Kura.
Rais Dkt,
Mwinyi amesema ni Wajibu wa Msingi wa kila Mwananchi Kuhakikisha Amani iliopo
inadumishwa wakati huu na Baada ya Uchaguzi Ili Nchi ipige hatua zaidi za
Maendeleo katika Nyanja tofauti.
Aidha
amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu Kuendeleza utaratibu wa Kuwasaidia Watu
wanaohitaji Misaada kama ilivyofanyika vema wakati wa Mwezi wa Ramadhani.
Halikadhalika
Rais Dkt, Mwinyi ameeeleza kuwa Mwenendo Mzuri uliotekelezwa wakati wa
Ramadhani unapaswa kuendelezwa kwa kiwango kile kile kwani bado makundi ya
Wanaohitaji Kusaidiwa yapo ndani ya Jamii.




0 Maoni