Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt.Hussein Ali Mwinyi
ataondoka nchini leo kuelekea Jijini London, nchini Uingereza kwa ziara ya
kikazi kuanzia tarehe 6 hadi 9 Aprili 2025 kwa ajili ya kushiriki katika
Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Trade &
Investment Summit 2025).
Katika ziara
hiyo Rais Dkt.Mwinyi matukio mengine atakayoshiriki ni kukutana na Viongozi
waandamizi wa Serikali ya Uingereza na Taasisi zake, atakutana na Diaspora wa Tanzania waliopo nchini
Uingereza, atakutana na Sir Tony Blair , Waziri Mkuu Mstaafu na Kiongozi wa
Tony Blair Institute (TBI), pia atakutana na wadau wa uwekezaji katika uchumi
wa bluu.
Halikadhalika
Rais Dkt.Mwinyi atakutana na wadau wa uwekezaji katika sekta ya utalii, filamu,
viwanda, nishati ikiwemo pia mafuta na gesi.
Vilevile Rais
Dkt.Mwinyi atashuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Wizara
ya Uchumi wa Buluu na Chuo Kikuu cha Kent kwa ajili ya utafiti wa kilimo cha
Mwani pamoja na MOU kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya
Perry Engineering ya Uingereza kuhusu usambazaji wa mbegu za mwani.

0 Maoni