Serikali itaendelea kuimarisha Mipango na Bajeti kwa ajili
ya ununuzi wa vifaa vya maabara na kemikali za maabara ili kuhakikisha
vinapatikana kwa uhakika na wakati kwa ajili ya ujifunzaji na kufundishia.
Haya yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa wakati wa kujibu hoja za wabunge kuhusu
mpango wa Serikali wa kupeleka vifaa vya maabara kwenye shule 26 za sayansi za
wasichana za mikoa, bila kuathiri mipango iliypowekwa ya upelekaji wa vifaa vya
maabara katika shule nyingine za sekondari nchini.
Amesema vifaa vya maabara kwa shule 486 vimenunuliwa katika
awamu mbili (2) na usambazaji wa awamu ya kwanza unahusisha shule 231, zikiwemo
shule 26 za sayansi za wasichana na hadi sasa shule 8 kati 26 za wasichana
zimepokea vifaa hivyo na usambazaji katika shule 18 zilizobakia unaendelea.
Amesema vifaa vya maabara na kemikali kwa awamu ya pili kwa
ajili ya shule 255 zilizobaki vinaendelea kupokelewa na kusambazwa na pia
Serikali imenunua na kusambaza kemikali za maabara katika shule za sekondari
231 ngazi ya kata.
Kuhusu kubuni chanzo cha kudumu cha fedha kwa ajili ya
ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini, Mchengerwa amesema
Serikali imekuwa ikitoa fedha za ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za
sekondari nchini kupitia Ruzuku ya Uendeshaji wa Shule.
Pia ununuzi wa vifaa vya maabara hufanyika kupitia
utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari
(SEQUIP), Mpango wa Lipa kulingana na Matokeo (EP4R) na michango ya wadau.
Hivyo, Mchengerwa amesema Serikali itaendelea kuimarisha
Mipango na Bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara na kemikali za
maabara ili kuhakikisha vinapatikana kwa uhakika na wakati kwa ajili ya
ujifunzaji na kufundishia.
Kuhusu hoja ya usimamizi na uendeshaji wa shule za mchepuo wa kiingereza katika halmashauri, Mchengerwa amesema Ofisi ya Rais - TAMISEMI imeipokea hoja hii na itafanya uchambuzi kwa kushirikiana na Wizara inayosimamia Sera ya Elimu ili kupata utekelezaji mzuri wahojahusika.
Na. OR-TAMISEMI
0 Maoni