Waziri Mkuu afungua kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya VETA

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kikataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Utoaji wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini na Miaka 30 ya VETA, Machi 18, 2025. Kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Syansi na Teknolojia, Profesa Adolf  Mkenda, waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dennis Londo, na kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda kuingia ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Mikutano cha Kikataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Utoaji wa Elimu ya Mafunzo ya Udundi Stadi inchini na Miaka 30 ya VETA, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Joshua Kingu mwanachuo kutoka Chuo cha VETA Kipawa jijini Dar es salaam, fani ya Mekatroniki alipotoa maelezo kuhusu mfano wa kiwanda unaotumika kufundishia,  alipotembelea banda la maonesho la Chuo hicho kabla ya   kufungua Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Utoaji wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini  na Miaka 30 ya VETA. Kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Abdallah Mohammed , Mkurugenzi wa  Vyuo na Mafunzo, Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar kuhusu hotipoti iliyotengenezwa kwa kutumia mti alipotembelea banda la manesco la  mamalaka hiyo  kabla ya kufungua Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Utoaji wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini na Miaka 30 ya VETA. Kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Fay Fashion Tanzania, Gregory (kushoto) kuhusu bidha mbalimbali zinazotengenezwa na  kampuni hiyo alipotembelea banda la maonesho la kampuni hiyo kabla  ya kufungua Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Utoaji wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi  Stadi inchini na Miaka 30 ya VETA. Kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Utoaji wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini  na Miaka 30 ya VETA, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Chapisha Maoni

0 Maoni