Rais Samia apokea Tuzo ya The Global Goalkeeper Award

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award kutoka kwa Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates, Dkt. Anita Zaidi kwenye hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025. Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha maendeleo kuelekea kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Mhe. Rais Samia amepewa Tuzo hiyo katika kipengele cha mapambano dhidi ya vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates Dkt. Anita Zaidi katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates kutoka Marekani Dkt. Anita Zaidi, Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Viongozi mbalimbali  kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kimataifa ya The Global Goalkeepers Award kutoka Taasisi ya Gates ya Marekani. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson.


Chapisha Maoni

0 Maoni