Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Nassoro Kuji amesisitiza
Ari na Kasi kubwa katika kutangaza vivutio vilivyopo katika Hifadhi za Taifa
Nchini.
Kamishna Kuji ameyasema hayo leo tarehe 01, Februari 2025
katika kikao kazi na Maafisa na Askari Uhifadhi waliopo katika Ofisi
Kiunganishi ya TANAPA iliyopo jijini, Dar es Salaam pamoja na Nyumba Kumbukizi
ya Mwalimu Nyerere iliyopo Magomeni.
Kupitia kikao kazi hicho Kamishna Kuji aliipongeza Ofisi
Kiunganishi pamoja na Nyumba Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa juhudi kubwa
zinazofanyika katika kujitangaza
na kuwataka kuongeza Ari na Kasi zaidi katika utangazaji na
utoaji wa taarifa katika ofisi mbalimbali na ili kupeleka elimu ya Uhifadhi na
Utalii na kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea katika maeneo yote ya Hifadhi
za Taifa.
“Jana kupitia uzinduzi wa takwimu za utalii na mapato
maarufu kama “T 506 USD” tulishudia mapinduzi makubwa yaliyochangiwa kwa kiasi
kikubwa na filamu ya “Tanzania :The Royal Tour” na “Amazing Tanzania” mapato
tunayoingiza sasa TANAPA ni “Amazing” kama ilivyo filamu aliyocheza Mhe.Rais
ambapo mapato yaliongezeka kutoka mapato ya billioni 57 wakati wa janga la
COVID -19 TANAPA ikafikisha mapato billioni 411, kwa mwaka wa fedha 2023/24 na
mpaka jana kwa mwaka wa fedha 2024/25
TANAPA imekusanya billioni 365 ikiwa ni miezi saba tu ya makusanyo”
alisema Kamishna Kuji.
“Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasaan, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ameshafanya sehemu yake ni jukumu letu watendaji tuliopo chini yake
kuendeleza Ari na Kasi kubwa aliyoanza nayo katika kunadi Utalii wetu na fursa
za uwekezaji zinazopatikana katika maeneo yote ya Hifadhi za Taifa niwatake
mkatekeleze hili kwa nguvu kubwa ili kufikia malengo ya Serikali iliyojiwekea.”
Naye, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Ofisi ya
Kiunganishi ya TANAPA, Dar es Salaam Neema Mollel, alimshukuru Kamishna wa
Uhifadhi kwa uongozi makini na katika kutoa
maelekezo yenye mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa TANAPA
inatekeleza majukumu yake ipasavyo na kuahidi
kuendeleza Ari na Kasi katika
kusimamia majukumu kwa weledi na ufanisi mkubwa.
Ofisi za Kiunganishi za TANAPA ni maalum katika kuendelea
kutangaza vivutio vya Utali, kuhamasisha watalii kutembelea maeneo ya vivutio
pamoja na kunadi fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa
nchini.
Kamishna Kuji anaendelea na ziara yake ya kikazi katika hifadhi za kanda ya mashariki.
Na. Edmund Salaho - Dar es Salaam
0 Maoni