CHADEMA acheni kuchukua vijana Tarime kufanya vurugu - Wasira

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema ni marufuku kwa vyama vya upinzani kuwatumia vijana kutoka mkoani Mara kama nguvu kazi ya kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali.

Wasira ametoa madaia hayo leo Februari 9, 2025, alipokuwa akizindua ofisi ya CCM Kata ya Nyakonga wilayani Tarime, mkoani Mara.

“CHADEMA wakitaka kufanya fujo mahali wanakuja kuchukua vijana Tarime.. wawapeleke yaani wao hawajui kupigana wanaojua kupigana ni wa Tarime, wanakwenda kufanya fujo wanafanya vijana wa Tarime kuwa majeshi ya kukodisha,” amesema Wasira.

Wasira amewataka vijana wasikubali kuchukuliwa na kutumika katika vurugu kwa kuwa wakienda huko hupigwa, kuumizwa na hata kupata ulemavu kisha kurudishwa Tarime wakiwa na hali mbaya.

Chapisha Maoni

0 Maoni