Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo
ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 29, 2024 huku likifuta
matokeo ya wanafunzi 67 wakiwemo watano walioandika matusi.
Matokeo hayo yametangazwa leo na Katibu Mtendaji wa NECTA,
Dkt. Said Mohammed jijini Dar es Salaam na kueleza kwamba kwa wanafunzi hao
walioandika matusi ni tatizo la maadili.
Kwa kuzingati maadili, matusi hayakubaliki katika chumba
cha mtiani na kila mahali, mwaka huu wametokea wanafunzi watano wameandika
matusi, amesema Dk Mohammed.
Kwa matokeo yote ya mtihani wa kidato cha nne bofya link hii hapa chini:-
https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/csee/CSEE2024/CSEE2024/indexfiles/index_h.htm
0 Maoni