Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza msamaha kwa wafungwa
1,548 ambapo kati yao wafungwa 22 wameachiliwa huru leo Desemba 09, 2024.
Taarifa
iliyotolewa leo imesema wafungwa 1,526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya
kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.
Kupitia taarifa
ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Serikali imesema msamaha huo wa Rais Samia
ni sehemu ya kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
“Ni
matarajio ya Serikali kuwa wafungwa walioachiliwa huru leo watarejea tena
katika Jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na
watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.” imesema taarifa hiyo.
0 Maoni