Rais Samia
Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo amemteua Prof.
Mpoki Ulisubisya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na
Ubongo Muhimbili (MOI).
Taarifa ya
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, imesema Rais Samia pia
amemteua Bi. Joyce Gideon Mapunjo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
0 Maoni