Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameirejesha Habari katika
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kumteua Prof. Palamagamba
Kabudi kuwa waziri wa wizara hiyo.
Taarifa ya
Ikulu aliyoitolewa leo na Katibu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka kufuatia
uteuzi wa viongozi mbalimali, Rais Samia amemteua, Gerson Msigwa kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa
Serikali.
Msigwa licha
ya kuwa Katibu Mkuu ameongezewa jukumu la Usemaji Mkuu wa Serikali akichukua
nafasi ya Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa
kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.
Rais Samia pia,
amemteua Mhe. Jerry Silaa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Dkt. Damas Ndumbaro ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria huku Mhe. Hamad
Masauni akiteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira). Uteuzi wa viongozi wote upo kwenye taarifa ya Ikulu hapo chini:-
0 Maoni