Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar.
Chuo Kikuu
cha Zanzibar kimemtunuku Shahada hiyo
ikiwa ni kutambua na kuthamini
Mchango wa Uongozi wake Unaoacha Alama na historia itakayokumbukwa wakati wote.
Hafla ya
kutunukiwa Shahada hiyo imefanyika jana tarehe 5 Desemba 2024 katika Viwanja
vya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wakati wa Mahafali ya 22 ya Wahitimu wa
mwaka 2024.
Shahada hiyo
ya Heshima ya Uchumi ametunukiwa
kuthamini Mchango wake na Mafanikio makubwa yaliofikiwa Zanzibar hususan Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo yaliopatikana
Kipindi kifupi cha Uongozi wake wa miaka minne
akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Rais Dk
Mwinyi amekishukuru Chuo hicho kwa kuthamini juhudi na kazi anazofanya kwa
ajili ya Maendeleo ya nchi.
Aidha Rais
Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Shahada hiyo aliotukuwa inaakisi kazi nzuri
inayoifanya na Serikali anayoiongoza na itamuongezea hamasa ya Maendeleo zaidi.
Kwa upande
mwingine Rais Dk.Mwinyi ameahidi kuienzi heshima hiyo na kuwahakikishia
wananchi kuendelea kuwatumikia kwa uwezo wake wote na sio mwisho wa safari bali
mwanzo wa hatua kubwa ya maendeleo yajayo.
0 Maoni