Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa leo Novemba 13, 2024 amefanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki
ambaye anamaliza muda wake Nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu, Ofisi ndogo
ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.
Katika
mazungumzo yao Mheshimiwa Majaliwa amemsihi Balozi Mehmet kuendelea kuwa balozi
mzuri wa Tanzania popote atakapokuwa sababu tayari anajua fursa za uwekezaji na
utalii zilizoko nchini.
Kwa upande
wake Balozi huyo ameshukuru Ushirikiano ambao ameupata kutoka Serikalini katika
kipindi chake jambo ambalo limechangia kuimarisha Ushirikiano baina ya nchi hizo
mbili.
Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha, Balozi wa Uturuki Nchini, Dkt.
Mehmet Gulluoglu baada ya mazungumzo kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu,
Magogoni jijini Dar es salaam, Novemba
13, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


0 Maoni