Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) inashiriki
maonesho ya utalii yajulikanayo kama 'My Tanzania road show'.
yanayoshirikisha
baadhi ya Taasisi za Wizara ya
Maliasili na Utalii (TAWA,TANAPA,NCAA) na Kampuni binafsi zinazojihusisha na utalii chini ya uratibu wa kampuni ya Kili Fair
iliyopo mkoani Arusha.
Maonesho ya Tanzania my Road show yamefunguliwa katika mji
wa Frankfurt nchini Ujerumani na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe.
Hassan Iddi Mwamweta tarehe 11 Novemba, 2024 na yatahitimishwa katika mji wa
Warsa, Poland tarehe 15 Novemba,2024 ambapo NCAA inawakilishwa na Afisa Utalii
Jemima Billiah.
Maonesho haya yanalenga kukutana na makampuni mbalimbali ya utalii katika nchi hizo na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania pamoja na maeneo ya uwekezaji.


0 Maoni