Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimejipanga na uchaguzi, mfano Mji wa Dodoma peke yake umeandikisha watu 628,000 na utekelezaji mzuri wa Ilani umefanyika kwa zaidi ya asilimia 90.
Dkt. Biteko ameeleza kutokana na uhamasishaji mkubwa wa
kujiandikisha kwenye daftrari la kupiga kura kufanywa vizuri “Hizi ndio
sababu za kupata ushindi kutokana na CCM kuwa na mtaji mkubwa wa wanachama...wakati wa uchaguzi tuikatae roho ya mgawanyiko na
tushikamane kwa ajili ya kujenga chama na na nchi yetu.”
Ameendelea kuwahimiza wana CCM kuwa chama chao ni chama kiongozi na kuwa waendelee kuhamasisha Watanzania kuendeleza misingi ya upendo, mshikamano na umoja sambamba na kuwa na upendo kwa vyama vingine vya siasa.

0 Maoni