Iran italipa kwa kitendo cha kuishambulia Israel- Netanyahu

  

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Iran italipa kwa kitendo cha kuishambulia kwa makombora 180 Israel siku ya Jumanne.

Makombora mengi yalifanikiwa kudhibitiwa, Mpalestina mmoja ameua katika eneo la Ukanda wa Magharibi, na shule eneo la kati la Israel na hoteli iliyopo Tel Aviv imeshambliwa.

Iran imesema mashambulizi hayo ni katika kujibu vitendo vya uchokozi vya Israel, ikiwamo vya kumuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Naseallah.

Jumanne, Israel ilianza mapigano ya kiwango kidogo ya ardhini kusini mwa Lebanon pamoja na kuendelea na mashambulizi ya anga Beirut.

Hezbollah wamesema wamewatimu wapiganaji wa ardhini wa Israel kusini mwa Lebanon Jumatano na wanaendelea kuishambulia kwa roketi.

Chapisha Maoni

0 Maoni