Kaka wa Michael, Tito Jackson afarika dunia

 

Tito Jackson, mmoja wa wanamuziki wa kundi la muziki wa pop la Jackson 5 na kaka wa marehemu Michael Jackson, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70.

Taarifa ya kifo chake zimeripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani hata hivyo chanzo cha kifo chake hakijabainika.

Tito alishiriki kutumbuiza pamoja na ndugu zake Jackie, Jermaine, Marlon na Michael, ambaye alifariki dunia 2009.

Hivi karibuni Tito alikuwa Jijini Munich kuelekea shoo ya kundi hilo waliyopanga kuifanya pamoja.

Chapisha Maoni

0 Maoni