Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa
Kilimanjaro wamenunua na kusambaza paipu kalavati kwa ajili ya kurudisha
mawasiliano kwenye madaraja yaliyokatika
wakati wa mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Meneja wa TARURA mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Nicholas
Francis amesema tayari wamepokea fedha za dharura takriban milioni 477 kwaajili
ya kununua vifaa vya kukabiliana na athari za mvua.
Paipu Kalavati ni
aina ya kalavati ambazo zinaweza kuwekwa
kwa haraka pale panapotokea barabara imekatika
na hivyo huwekwa kwa urahisi na haraka ili kuweza kurudisha mawasiliano
kwa wananchi na kuweza kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.
Mhandisi Francis amesema hadi sasa paipu kalavati hizo zimeshasambazwa katika wilaya zote saba ikiwemo Same, Mwanga, Rombo,Manispaa ya Moshi,Moshi Vijijini,Hai pamoja na Siha.

0 Maoni