Rais Samia aongeza bajeti ujenzi wa barabara za Ruangwa- Majaliwa

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza bajeti kwa ajili ya ujenzi wa barabara za ndani katika wilaya ya Ruangwa kutoka shilingi Bilioni 1 hadi shilingi bilioni 4.8

“Niwape Siri, Rais Dkt. Samia ametuunganisha  Masasi na Ruangwa kupitia ujenzi wa barabara ya Nanganga-Ruangwa na Km 38 zimejengwa pia ametupa fedha kwa ajili ya kuunganishwa Ruangwa na Nachingwea kwa kiwango cha lami,” alisema Mhe. Majaliwa.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amesema hayo leo Desemba 29,2023 wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Litama, Ruangwa mkoani Lindi.

Chapisha Maoni

0 Maoni