Kombora la Urusi laua watu wanne Ukraine

 

Kombora la roketi la Urusi limepiga jengo la makazi magharibi mwa mji wa Ukraine, Lviv, na kuua watu wapatao wanne, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine amesema.

Waziri huyo Ihor Klymenko, ameongeza kuwa watu wengine 32, wamejeruhiwa katika kile Meya wa Lviv alichokiita moja ya mashambulizi makubwa yaliyowalenga raia katika makazi yao.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameapa kulipiza kisasi kwa shambulizi hilo la usiku lililofanywa na “magaidi wa Urusi”.

Chapisha Maoni

0 Maoni