Ahmed Ally atuma salamu za pole kwa Yanga


 Meneja wa mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally baada ya kumalizika kwa fainali ya CAFCC na USM Alger kutangazwa mabigwa dhidi ya Yanga ametuma salamu.


Katika salamu zake za pole kwa watani wake Yanga Ahmed ameandika kupitia mtandao wa twita kwa mtindo wa maswali “Wamejitahidi nini?? Wamekufa kiume gani?! Wamepambana kitu gani?”


Ameongeza kuinanga Yanga kwa kuandika “Yaani kufungwa na timu ambayo inashika nafasi ya 10 kwenye ligi yao ni kujitahidi, Kufungwa na timu ambayo ni ngeni ni kwenye mashidano ya Afrika ni kufa kiume” 



Akahitimisha “Hapo wameambulia fedheha tuu, wamecheza na timu wanayolingana nayo hakuna cha kujitahidi” huku  katika ukurasa wake wa instagram aliandika “tumefarijika” ambapo alijibiwa na shabiki akimpa ushauri kuimarisha timu na kutoishia robo fainali pekee.


Ikumbukwe kabla ya Yanga kwenda Algeria Msemaji wake Ally Kamwe alionesha kurusha vijembe vingi mtandaoni haswa kwa watani wake.

Utani huu wa jadi haubadili uzalendo kwa wawakilishi wa taifa bali kuendeleza tambo katika mchezo pendwa wa mpira wa miguu.


Katika fainali hiyo Kipa wa Yanga  Diarra ameonekana mwamba, haswa kwa kupangua penati ya USM Alger na zaidi anarudi nyumbani akiwa ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo wa fainali za CAFCC.

Chapisha Maoni

0 Maoni