Mhubiri Ezekiel Odero wa kanisa la New Life Prayer Centre wa nchini Kenya amekamatwa na vyombo vya usalama na atashtakiwa kwa tuhuma za mauaji ya waumini wake.
Odero amekamatwa leo asubuhi akiwa nyumabni kwake Mavueni, Kaunti ya Kilifi, na kuhojiwa makao makuu ya upelelezi mkoa, Mombasa kwa tuhuma za kanisa lake pia linahubiri kujiua.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kenya Kithure Kindiki, amesema Odero anahusishwa na makosa ya mauaji ya watu wengi.
Pia kukamatwa kwake kumefuatia saa chache tu kupita tangu kufungwa kwa kanisa lake kubwa lililopo Mavueni katika kaunti ya Kilifi.
Waziri Kindiki amesema kwamba watu wapatoa 100 waliokutwa katika eneo la mhubiri Odero wanashikiliwa kwa ajili ya kuisaidia polisi.
Kindiki amesema wamechukua uamuzi wa kumkamata mhubiri huyo baada ya tuhuma za kuwapo kwa matukio ya vifo katika eneo lake.
Odero anakuwa kiongozi wa pili wa kanisa Kenya kukamatwa kwa tuhuma za mauaji ya waumini wake baada ya Mchungaji Paul Mackenzie ambaye anashikiliwa kwa mauaji ya waumini wake 98.
0 Maoni