Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na uhamisho huo ni kama ifuatavyo:
A) Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa
Uteuzi
(i) CP Salum Rashid Hamduni, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza;
(ii) Bw. Alexander Pastory Mnyeti ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita;
(iii) Bw. Stanslaus Haroon Nyongo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; na
(iv) Bw. Jumanne Abdallah Sagini ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Uhamisho
(i) Mhe. Martine Reuben Shigela amehamishwa kutoka Mkoa wa Geita kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara;
(ii) Mhe. Said Mohamed Mtanda amehamishwa kutoka Mkoa wa Mwanza kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Bw. Anamringi Macha ambaye amestaafu;
(iii) Mhe. Abubakar Mussa Kunenge amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Mhe. Kunenge anachukua nafasi ya Bw. Jabiri Omari Makame ambaye atapangiwa majukumu mengine;
(iv) Mhe. Beno Moris Malisa amehamishwa kutoka Mkoa wa Mbeya kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Mhe. Malisa anachukua nafasi ya Bw. Paul Matiko Chacha ambaye aliteuliwa kuwa Katibu wa NEC – Idara ya Organaizesheni ya Chama cha Mapinduzi (CCM);
(v) Mhe. Adam Kighoma Malima amehamishwa kutoka Mkoa wa Morogoro kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Mhe. Malima anachukua nafasi ya Bi. Zainab Telack ambaye amestaafu; na
(vi) Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
B) Uteuzi na Uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa
Uteuzi
(i) Bw. Richard Marcellino Kayombo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.
Uhamisho
(i) Bw. Balandya Mayuganya Elikana amehamishwa kutoka Mkoa wa Mwanza kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya;
(ii) Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga amehamishwa kutoka Mkoa wa Singida kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza;
(iii) Bi. Pili Hassan Mnyema amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga; na
(iv) Bw. Rodrick Lazaro Mpogolo amehamishwa kutoka Mkoa wa Mbeya kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida.
Aidha, uapisho wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
Bakari S. Machumu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

0 Maoni