Prof. Muhongo awaalika Wanasayansi kushiriki mkutano wa 16 wa AAS

 

Wanasayansi, watafiti, wabunifu na watunga sera barani Afrika, wakiwemo wanafunzi, wamehimizwa kushiriki Mkutano wa 16 wa Baraza la Uongozi la Wanazuoni wa Sayansi Afrika (AAS), unaolenga kuwakutanisha wadau mbalimbali katika nyanja za sayansi, utafiti na ubunifu. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Makamu wa Rais wa AAS Kanda ya Afrika Mashariki, Prof. Sospeter Muhongo, Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo imekamilisha maandalizi ya waraka wa pili unaoeleza kwa kina taarifa muhimu kuhusu mkutano huo, ikiwemo taratibu za ushiriki. 

Muhongo amewaalika wanasayansi na watafiti pamoja na wenzao kuwasilisha machapisho ya utafiti na kujisajili kushiriki mkutano huo kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa katika waraka huo wa pili. 

Amesisitiza kuwa wanawake na vijana wanaofanya shughuli za kisayansi na utafiti, wakiwemo wanafunzi, pamoja na wabunifu na watunga sera katika nyanja zote, wanahimizwa kushiriki katika mkutano huo wa kimataifa.

Chapisha Maoni

0 Maoni