KUELEKEA AFCON 2027: TARURA yaongeza kasi ujenzi wa barabara Dar es Salaam

‎Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amesisitiza kuongezwa kwa kasi, ubora na usimamizi madhubuti wa miradi ya barabara inayotekelezwa katika mkoa wa Dar es Salaam ili kuhakikisha Tanzania inakuwa tayari kupokea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

‎Mhandisi Seff ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa na TARURA mkoani Dar es Salaam ikiwemo mikataba minne inayolenga kuimarisha miundombinu katika maeneo yatakayohudumia mashindano hayo ambapo maeneo ya kazi ya mikataba hiyo yalikabidhiwa rasmi kwa wakandarasi tarehe 2 Agosti 2026 na sasa kazi zinaendelea.

‎Katika ziara hiyo, Mhandisi Seff amekagua Uwanja wa Benjamin Mkapa na maeneo yanayouzunguka uwanja huo katika Manispaa ya Temeke ambapo amefanya kikao cha tathmini na timu ya mradi na kujionea hali ya barabara za kuingia uwanjani, maeneo ya maegesho pamoja na barabara za kuunganisha uwanja huo.

‎Aidha, ametembelea barabara ya Dahomey iliyopo Manispaa ya Kinondoni ambapo alijionea kazi za uchimbaji, ujazaji, uwekaji wa mawe ya kando ya barabara na maandalizi ya tabaka la msingi zikiendelea, huku alama za tahadhari na usalama zikiwa tayari zimewekwa.

‎Katika hatua nyingine, Mhandisi Seff amekagua maeneo yanayoendelea kufanyiwa uhamishaji wa miundombinu ya huduma katika Manispaa ya Temeke ikiwemo nguzo na nyaya za umeme, mabomba ya maji na miundombinu ya mawasiliano ili kupisha ujenzi na upanuzi wa barabara pamoja na uboreshaji wa hifadhi za barabara.

‎Akizungumza katika kikao na timu ya mradi kilichowahusisha wakandarasi Nyanza, Controlled Blasting na Plattnum  pamoja na Wahandisi Washauri, Mhandisi Seff ametoa maelekezo ya kuhakikisha kazi zote za udongo zinakamilishwa kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua unaotarajiwa kuleta changamoto kubwa za utekelezaji.

‎"Kazi zote za udongo zinapaswa kukamilika kabla ya Septemba 30, 2026. Hatutaki mvua ziwe sababu ya kuchelewesha utekelezaji wa miradi hii",  amesisitiza.

‎Vilevile, amerejea agizo lake la awali la kuongeza muda wa kufanya kazi saa 24 katika maeneo yote yanayohitaji kasi zaidi kwa kuongeza nguvu kazi, mitambo na rasilimali nyingine muhimu ili kuhakikisha miradi inakwenda sambamba na ratiba iliyowekwa.

‎Mhandisi Seff amesisitiza kuwa ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua na miundombinu ya kupitisha maji upewe kipaumbele akieleza kuwa mifumo bora ya majitaka na maji ya mvua ni muhimu katika kulinda uimara wa barabara na kuongeza muda wa matumizi ya miundombinu hiyo.

‎Pamoja na kusisitiza kasi, Mtendaji Mkuu amewataka Wakandarasi, Wahandisi Washauri na wataalamu wote wanaosimamia miradi hiyo kuzingatia ubora, weledi na thamani ya fedha za umma akisisitiza kuwa kasi ya utekelezaji haiwezi kuwa sababu ya kushusha viwango vya usanifu na ujenzi.

‎"AFCON 2027 ni fursa ya kihistoria kwa nchi yetu. Tunachojenga si miundombinu ya maonesho ya siku 30 bali tunajenga miundombinu ya kudumu itakayowanufaisha watanzania kwa miaka mingi ijayo hivo ubora ni suala la lazima", amesema Mhandisi Seff.

‎Katika hatua nyingine, Mtendaji Mkuu amekagua maendeleo ya uhamishaji wa miundombinu ya huduma unaofanyika kwa ushirikiano kati ya TARURA, TANESCO, DAWASA na watoa huduma za mawasiliano ambapo kazi za kuhamisha nguzo za umeme, mabomba ya maji na miundombinu ya mawasiliano zinaendelea ili kupisha ujenzi wa barabara na uboreshaji wa hifadhi ya barabara.

‎Amesisitiza kuwa taasisi zote zinazohusika ziongeze kasi ili kuepusha ucheleweshaji wa miradi na kuzitaka mamlaka za huduma kuwapa wananchi taarifa mapema pale huduma zitakapokatizwa kwa muda kutokana na kaMtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amesisitiza kuongezwa kwa kasi, ubora na usimamizi madhubuti wa miradi ya barabara inayotekelezwa katika mkoa wa Dar es Salaam ili kuhakikisha Tanzania inakuwa tayari kupokea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

‎Mhandisi Seff ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa na TARURA mkoani Dar es Salaam ikiwemo mikataba minne inayolenga kuimarisha miundombinu katika maeneo yatakayohudumia mashindano hayo ambapo maeneo ya kazi ya mikataba hiyo yalikabidhiwa rasmi kwa wakandarasi tarehe 2 Agosti 2026 na sasa kazi zinaendelea.

‎Katika ziara hiyo, Mhandisi Seff amekagua Uwanja wa Benjamin Mkapa na maeneo yanayouzunguka uwanja huo katika Manispaa ya Temeke ambapo amefanya kikao cha tathmini na timu ya mzi za ujenzi.

‎Kwa ujumla hali ya utekelezaji wa miradi inaonesha kuwa wakandarasi wote wapo maeneo ya kazi na shughuli za maandalizi, uondoshaji wa vikwazo, kazi za udongo pamoja na uhamishaji wa miundombinu zinaendelea sambamba na hatua za kuimarisha usalama kwa wafanyakazi na watumiaji wa barabara.



Chapisha Maoni

0 Maoni