Rais Samia Suluhu Hassan, amesema penye siasa za chuki na mivutano, maendeleo hutoweka, huku panapokuwa na siasa za staha na maridhiano, maendeleo hupata nafasi na kuchanua.
Amesema hatua iliyofikiwa Zanzibar,
ni makubaliano ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuanza
mazungumzo ya mustakabali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais
Samia ameyasema hayo visiwani Zanzibar leo, Alhamisi Julai 9, 2026
alipohutubia wakati wa hafla ya utiaji saini Tamko la Pamoja la
Maridhiano ya Kisiasa Zanzibar.
Ametoa wito wa kuheshimiwa kwa
makubaliano hayo na kuendeleza mazungumzo kwa uwazi na kuaminiana,
huku misingi ya umoja, amani, usalama na utulivu wa Taifa
ukizingatiwa.
Ameeleza hekima iliyoonyeshwa ikalindwe kwa
matendo mema ya kesho na imani iliyojengwa kwa muda mrefu isiangushwe
kwa maneno au mienendo isiyo na tija.

0 Maoni