WATANZANIA
wanaitakia mema Tanzania wanapaswa kuendelea kutete amaridhiano na
amani na kukumbuka kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan, alishahakikishia Watanzania kuwa msimamo wake wa
kuongoza nchi kupitia falsafa ya 4R ambayo ni Maridhiano,
Ustahimilivu, Mageuzi, na Kujenga Upya Taifa haujabadilika.
Tukumbuke kwamba akipokea ripoti ya Tume ya Kuchunguza
Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kutoka kwa
Jaji Othman Chande mnamo Aprili 23, 2026, Rais Samia alieleza kuwa
yeye bado ni yuleyule aliyeingia madarakani na nia ya kuleta
maridhiano ya kweli.
Alisisitiza kuwa anachoomba kutoka kwa
viongozi na wananchi ni ushirikiano wa dhati katika kutekeleza
falsafa hiyo, akibainisha kuwa umoja ni nguzo muhimu katika kuvuka
changamoto zilizojitokeza wakati wa mchakato wa uchaguzi
uliopita.
Ni kweli kua falsafa hiyo ya 4R imekuwa ikitekelezwa
kwa vitendo tangu mwanzo wa utawala wake kupitia hatua mbalimbali za
kuimarisha demokrasia na haki za binadamu nchini.
Ikumbukwe
kuwa Rais Samia amekuwa kiongozi aliyefungua milango ya mazungumzo na
vyama vya upinzani, kuwaruhusu wanasiasa waliokuwa nje ya nchi
kurejea, na kutoa uhuru mkubwa kwa vyombo vya habari na mikutano ya
kisiasa. Aidha, amefanya mageuzi makubwa ikiwemo kuondoa matumizi ya
nguvu katika ukusanyaji wa kodi, kugharamia matibabu ya viongozi wa
upinzani kama Tundu Lissu, na kuanzisha Tume ya Hakijinai ili
kuboresha mfumo wa haki nchini.
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu
wa 2025, Rais alionyesha uthabiti wake kwa kufuta utaratibu wa
wagombea kupita bila kupingwa na kuondoa wakurugenzi wa halmashauri
katika usimamizi wa uchaguzi ili kuongeza uwazi.
Licha ya
kuwepo kwa kasoro na vurugu zilizoripotiwa katika uchaguzi wa Oktoba
29, 2025, Rais Samia anaamini kuwa suluhu pekee ya kudumu ni
kuendelea na njia ya maridhiano badala ya uhasama. Maono yake ni
kuona Watanzania wanabaki kuwa wamoja na wenye utulivu ili waweze
kuendelea na shughuli zao za maendeleo huku wakijenga taifa lenye
misingi imara ya haki na ustahimilivu.
#UmojaWetuNdiyoNguvuYetu
#turidhiane

0 Maoni