Biashara haina itikadi ya vyama, Amani na utulivu ndio mpango mzima

WAKINA mama wanaojihusisha na uuzaji wa mbogamboga Jijini Dar es Salaam, Sikitu Bakari na Angela Mwaikambo, wameeleza kuwa utulivu wa mazingira ya biashara ni nguzo muhimu inayowezesha shughuli zao kufanyika kwa ufanisi na kuwaletea kipato cha uhakika.

Akizungumza, Sikitu Bakari amesema kuwa biashara ya mbogamboga inategemea sana amani na utulivu, kwani wateja hupatikana kwa urahisi pale mazingira yanapokuwa salama na tulivu, hali inayochochea mzunguko wa fedha.

Amesisitiza kuwa vurugu au migogoro ya aina yoyote huathiri moja kwa moja biashara, kwa kupunguza idadi ya wateja na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara wadogo.

Kwa upande wake, Angela Mwaikambo amesema kuwa biashara haina misingi ya vyama vya kisiasa, hivyo ni muhimu kwa wafanyabiashara na wateja kujiepusha na kuingiza itikadi za kisiasa katika shughuli za kiuchumi.

“Hapa akija mteja namtajia bei ya nyanya, vitunguu, biringanya, karoti na pilipili hoho sijui ni wa chama gani na yeye hajui mimi ni wa chama gani..na wala hatuulizani vyama, nina muuzia anaondoka,” alisema Mwikambo.

Ameongeza kuwa bei za mgogamboga haziangalii itikadi za vyama, bali huamuliwa na hali ya soko, upatikanaji wa bidhaa na gharama za uzalishaji na usafirishaji.

Wauzaji hao wamewataka wananchi kudumisha amani na mshikamano, wakisisitiza kuwa utulivu wa nchi una mchango mkubwa katika kukuza biashara na kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla.

#SisiNiWamoja




Chapisha Maoni

0 Maoni