Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mashindano ya Kimataifa ya Quraan Tajweed ni jukwaa muhimu la kuimarisha mapenzi ya Quraan, kukuza vipaji vya vijana na kuitangaza Tanzania kimataifa.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika fainali ya Mashindano ya 22 ya Kimataifa ya Qurani - Tajweed yaliyoandaliwa na Taasisi ya Khidmatul Quran Tanzania na kuwakutanisha washiriki kutoka mataifa 12, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre.
Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza taasisi hiyo kwa kuandaa mashindano yenye hadhi ya kimataifa, akisema yanajenga kizazi chenye maadili na hofu ya Mwenyezi Mungu. Aidha, amewashukuru wadhamini hususan CRDB Bank kupitia kitengo cha Al Barakah na kutoa wito wa kuchangia ujenzi wa Skuli ya Quraan na Kituo cha masomo ya Dini.




0 Maoni