Wakati
Dunia ikikimbilia kwenye Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, Tanzania imechagua njia
ya kipekee: Kugeuza viganja vya vijana wake kuwa viwanda vya teknolojia badala
ya kuwa vyanzo vya malalamiko.
Serikali
ya Awamu ya Sita, chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka mezani
mwarobaini wa kudumu wa changamoto ya ajira kupitia uwekezaji mkubwa katika
sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA).
Uamuzi
wa kuanzisha "Open Coding Schools" na kufufua vituo vya kimkakati
kama Ilonga na Sasanda, siyo tu mpango wa elimu, bali ni mkakati wa kiusalama
na kiuchumi kuelekea Dira ya Maendeleo 2050. Huu ni ujumbe wa wazi kwa vijana:
Zama za kusubiri bahasha za bahati zimepita; sasa ni zama za kuandika misimbo
(Coding) inayotatua matatizo ya jamii.
Coding:
Zaidi ya Teknolojia, ni Uhuru wa Kiuchumi
Fikiria
kijana anayetumia saa tano mtandaoni. Je, anatumia muda huo kupokea maelekezo
ya "wanaharakati waovu" wanaolenga kuchoma moto nchi yake na kubomoa
amani? Au anatumia muda huo kusoma Python, Java, au Mobile App Development?
Coding
inampa kijana uwezo wa kutengeneza mifumo inayounganisha mkulima wa kijijini na
masoko ya kidunia. Inamfanya kijana wa Songwe au Kilimanjaro kutengeneza
suluhisho (Apps) za kukodisha vifaa vya ujenzi au kusimamia mifumo ya afya.
Hapa, kijana hahitaji 'connection' ya kujuana na mtu; anahitaji akili,
kompyuta, na utulivu wa nchi.
Amani
Ndiyo 'Server' ya Maendeleo
Wataalamu
wa usalama na uchumi wanabainisha kuwa bila amani, hakuna intaneti, hakuna
utalii, na hakuna mikopo ya asilimia 10. Kijana anayejitambua hawezi kukubali
kutumika kama 'kiberiti' cha kuwasha moto nchi yake. Akijua kuwa amani
ikivurugika, mnyororo mzima wa uchumi unakatika—kuanzia kwa Mama Lishe
anayepoteza wateja hadi kwa mtaalamu wa Coding anayepoteza soko la kimataifa.
Kama
alivyowahi kunukuliwa Askofu Dkt. George Pindua, "Tupambane na chochote
kinachotishia misingi yetu ya umoja." Uzalendo wa karne ya 21 ni kulinda
taswira ya Tanzania mtandaoni na kuitumia teknolojia kukuza pato la taifa,
badala ya kuwa mshabiki wa propaganda zinazofadhiliwa na washindani wa taifa
letu.
Nafasi
ya Uwekezaji na Fursa Mezani
Tanzania
imejipanga kuwa kitovu cha TEHAMA (ICT Hub) Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa
sasa, bilioni za shilingi ziko mezani kupitia mikopo na mifuko ya ubunifu
(Innovation Funds). Kituo cha TEHAMA (ICTC) kinatoa fursa kwa vijana kugeuza
mawazo (Startups) kuwa mamilioni ya dola.
Kwa
nini uwekeze kwenye Coding sasa? La kwanza kabisa kuna soko la uhakika:
Mahitaji ya mifumo ya kidijitali yanazidi kukua kila uchao.Pili kujiajiri:
Unakuwa bosi wa akili yako na muda wako na tatu kulinda Taifa: Unatumia
teknolojia kuelezea vivutio vya utalii na fahari ya Tanzania, ukishinda
propaganda za maadui.
Wito
kwa Kijana wa Kitanzania
Dira
ya 2050 haitatimizwa na miujiza, bali na vijana wanaoamua kuwa sehemu ya
suluhisho. Badala ya kutumika kama chombo cha chuki mtandaoni, geuza simu yako
kuwa darasa. Ingia kwenye "Open Coding Schools", jifunze uandishi wa
programu, na uwe Bill Gates ajaye wa Kitanzania.
Umaskini
si kisingizio tena kama una uwezo wa kupata mtandao. Tumia amani iliyopo, tumia
mikopo ya serikali, na tumia Coding ili kuyapatia maisha yako. Tanzania yenye
uchumi wa kidijitali inaanza na msimbo (code) mmoja utakaoandika leo!

0 Maoni