Taasisi za Kiislamu Tanzania zimetoa tamko kali la msimamo kuhusu vurugu zilizosababisha hasara kubwa ya watu na mali nchini, huku zikimuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine waliochaguliwa.
Tamko hilo lililosomwa na Shehe
Issa Othman Issa, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa BAKWATA, limetoa wito wa
maridhiano huku likionya dhidi ya kuwatunuku waliosababisha machafuko.
Alisema tangu awali viongozi wa
Taasisi za Kiislamu walifanya juhudi kubwa kuhimiza amani kabla ya uchaguzi na
wamesema kazi hiyo wataendelea nayo kwa maslahi mapana ya taifa. Walionya,
"Kamwe wasionekane wajinga kwa kuendelea kuhimiza amani ambayo ni kwa
faida ya Watanzania wote."
Wawataka waislamu kote nchini na
watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao kuendelea kudumisha amani na kama
kundi lolote likiona kuna haja ya kudai,
kuomba au matakwa yoyote ni wajibu wa wanaodai kuzingatia kuwa ni vyema
mazungumzo yaendelee na kamwe kwenye vurugu kinachopatikana ni hasara tu.
Maridhiano na Pongezi
Tamko hilo lilitamatika kwa mambo
muhimu matatu, ikiwa ni pamoja na maombi mahususi kwa Serikali na pongezi kwa
uongozi wa nchi:
Maridhiano ya Kisiasa:
Taasisi za Kiislamu zimeiomba
Serikali kutafuta fursa ya suluhu na maridhiano, lakini zimetoa onyo kali
kwamba maridhiano hayo hayapaswi kuwa zawadi kwa walioleta fujo.
Pongezi:
Wamempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan na viongozi wengine waliochaguliwa kwa kumaliza salama mchakato
wa uchaguzi.
Uchaguzi wa Amani:
Viongozi wa dini na wanasiasa
wametakiwa kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuacha kuwahamasisha vijana kufanya
vurugu. Badala yake, wamehimiza kuwa haki yoyote inayotafutwa, idaiwe kwa njia
ya amani na mazungumzo, kwani vurugu haziwezi kuleta haki bali zitaleta maafa.
Msimamo Mzito Kuhusu Vurugu na
Uwajibikaji
Akisoma tamko hilo, Shehe Othman
alisisitiza kuwa jukumu la kuhimiza amani wataliongoza daima, akionya kusiwepo
na kundi linalojiona lina haki zaidi ya kusikilizwa kuliko wengine.
Uchaguzi wa Amani:
Viongozi hao wameendelea kuhimiza
Waislamu kote nchini na Watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao kuendelea
kudumisha amani. Wamesisitiza kuwa kundi lolote likiona kuna haja ya kudai au
kuomba matakwa yoyote, ni wajibu wake kuzingatia kuwa mazungumzo yaendelee na
kamwe kwenye vurugu kinachopatikana ni hasara tu.
Wito kwa Serikali:
Taasisi za Kiislamu zimeitaka
Serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kuhamasisha vurugu
zilizosababisha maumivu na hasara kubwa ya watu na mali, ili hatua za kisheria
zichukuliwe.
Msaada kwa Waathirika:
Pia, wameiomba Serikali
kuwasaidia walioathirika na walioumizwa kwa bahati mbaya wakati
wa machafuko hayo.

0 Maoni