Jeshi la Polisi nchini limetangaza mafanikio makubwa katika kushughulikia matukio ya kihalifu nchini, likisisitiza kuwa kwa sasa lina uwezo zaidi na linafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu kutokana na kuwezeshwa na Serikali.
Akizungumza chombo kimoja cha habari hapa nchini, kuhusu
kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David
Misime alifafanua kuwa ripoti za upotevu na utekaji hazipuuzwi na kwamba juhudi
kubwa zimekuwa zikifanya kufichua uhalifu huo na kuwatia mbaroni wahusika.
"Si
kweli kwamba tukipatiwa ripoti hatuzifanyii kazi. Tunazifanyia kazi.
Kiutekelezaji ni suala la muda tu; halafu mtuhumiwa atakamatwa," alisema.
Msemaji huyo alibainisha kuwa kuna matukio zaidi ya
86 yaliyokuwa na maelezo ya kupotea na kutekwa ambayo yameshughulikiwa. Katika
matukio hayo, watu kadhaa wamekamatwa na kufikishwa mahakamani, huku wengine
wakiwa tayari wamepewa hukumu.
Alisema vyombo vya habari vinapaswa kuwa na
kumbukumbu katika matukio hayo na kazi iliyofanywa na jeshi la polisi kwa kuwa
ndio wanaopelekewa taarifa kwa ajili ya kuzifikisha kwa umma kuonesha maendelea
ya mashauri mbalimbali yaliyokuwa yanatafutiwa ufumbuzi na jeshi hilo.
Katika mazungumzo yake aliyataja baadhi ya mashauri ambayo yalikuwa na dhana ya kupotea
au kutekwa na polisi baada ya upelelezi ikabaini kwamba kulikuwa na uhalifu
kutokana na imani za kishirikina, wivu wa mapenzi na mauaji yanayohusiana na
mirathi au biashara.
Misime aliyataka mauji ya watu 11 Singida, mauaji ya
mfanyabiashara Njombe na mauaji ya mke yaliyofanywa na mume huko Kigamboni.

0 Maoni