Mwanaharakati wa mitandaoni, Mange Kimambi,
amejikuta katika hali ya aibu baada ya maandamano aliyoyatisha nchini Marekani
tarehe 17 Oktoba 2025 kushindwa kuvutia umati kama alivyotarajia.
Licha ya kufanya kampeni kubwa kupitia mitandao ya
kijamii na kutoa ahadi kwamba Watanzania wengi wanaoishi Marekani wangekwenda
kumuunga mkono, tukio hilo lilishuhudia mahudhurio duni, hali iliyoashiria
ukosefu wa uungwaji mkono wa kweli.
Tukio hilo limebainisha ukweli kwamba sauti kubwa
mtandaoni si kigezo cha ushawishi katika uhalisia. Mange, ambaye
amejitambulisha kwa muda mrefu kama
msemaji wa wananchi, inaonekana hakusoma kwa
usahihi mtazamo na hisia za Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kuhusu
ajenda zake za kisiasa na kijamii.
Wengi wa Watanzania wanaoishi Marekani wameonekana
kuchoshwa na siasa za majukwaa ya mtandao na badala yake wanaunga mkono
mabadiliko ya kweli yanayoendelea kufanywa nchini Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa ujumla, kushindikana kwa maandamano hayo ni somo
muhimu kwa wanaharakati wote kwamba nguvu ya maneno mtandaoni haiwezi kuchukua
nafasi ya vitendo halisi.
Ni wazi kwamba watanzania wanatakiwa kutafakari kwa
kina kile kilichotokea Marekani na uhalisia wa mambo kwani wao ndiyo hasa wanaoshuhudia
maendeleo yanayoendelea kuonekana kuliko hao walioko nje ya Nchi.

0 Maoni