Wanu Ameir aahidi kuinua kilimo cha mwani Makunduchi

 

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Makunduchi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Wanu Hafidh Ameir akiwa katika Viwanja vya Jamhuri vilivyopo Makunduchi, Kusini Unguja jana tarehe 26 Septemba, 2025 amenadi Sera zake kwa kwa Wanamakunduchi na kuomba ridhaa kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 nchi nzima.

Aidha, Mgombea Ubunge Jimbo la Makunduchi, Wanu Hafidhi Ameir amehutubia wananchi na kuweka bayana vipaumbele kadhaa ikiwemo;

Kwanza; Kujenga ukuta wa Hospitali ya Wilaya Makunduchi

Pili; Kuwawezesha kifedha Wanawake wakulima wa zao la Mwani

Tatu; Kuwanunulia Gari  Wanawake Wakulima wa zao la Mwani ambalo watalitumia kwenye shughuli zao za Mwani

Vilevile, Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Makunduchi, Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman kwenye mkutano wa kampeni za CCM pamoja na wagombea wengine wamenadi sera zao kwa wananchi na kuomba kura ili kupata ridhaa ya kuchaguliwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Pamoja na mambo mengine, Wanu Hafidh Ameir amewaomba wana Makunduchi wote kumpigia kura Mgombea Urais Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan; Mgombea Urais Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi; Mgombea Ubunge Makunduchi; Mgombea Uwakilishi Makunduchi na Madiwani wa Wadi za Makunduchi.

#MakunduchiMpya

#MakunduchiNiYetu

#OktobaTunatiki

#KaziNaUtu

#TunasongaMbele

Chapisha Maoni

0 Maoni