Mkutano wa Katibu wa
Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla ulipaswa kufanyika
jana saa 11 jioni ya Julai 28, sasa utafanyika leo saa 6:00 mchana Julai
29, 2025.
Taarifa iliyotolewa leo imesema Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM CPA Amos Makalla atafanya mkutano na waandishi wa habari kuanza ifikapo saa 6:00 mchana.
Mabadiliko hayo yamekuja baada ya waandishi wa habari kukaa katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM Dodoma jana kwa zaidi ya saa 10 wakisubiri taarifa kutoka kwa Makalla.
0 Maoni