Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania (TAWA) imepokea Tuzo ya shukrani kutoka kwa Taasisi isiyo
ya Serikali inayojulikana kama Foundation for Disabilities Hope (FDH) iliyopo
Mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hiyo jana Julai 14,2025, katika Ofisi za Makao Makuu ya TAWA
zilizopo Mkoani Morogoro, Kaimu Kamishna wa TAWA, Mlage Kabange alisema TAWA
imekuwa ikishirikiana na FDH katika utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya
uhifadhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuilinda rasilimali ya
wanyamapori na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya hifadhi.
Sambamba na hilo,
Kamishna Kabange alisema katika kuhakikisha jamii inanufaika na shughuli za
uhifadhi, TAWA imeweka utaratibu maalumu wa kuruhusu wananchi kufanya shughuli
za uvuvi na ufugaji nyuki katika baadhi ya maeneo inayosimamia ili kuruhusu
wananchi kujipatia kipato kutoka katika uhifadhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya FDH, Maiko Salali aliishukuru TAWA kwa ushirikiano wanaoutoa kwa
Taasisi yao, Aidha, alisema FDH imekuwa ikitambua mchango wa Taasisi mbalimbali
zinazosaidia jamii ya watu wenye ulemavu na TAWA ni miongoni mwa Taasisi kinara
ambayo imekuwa ikitoa msaada unaowasaidia makundi hayo kufikia malengo na
kutatua changamoto mbalimbali.
Bw. Salali aliongeza kuwa
FDH imeguswa na jitihada zinazofanywa na
TAWA za kuweka kipaumbele kundi la watu wenye ulemavu hivyo Tuzo hii ni
kutambua mchango wa TAWA kwa makundi ya watu wenye ulemavu.
Sambamba na hilo, Bw.
Salali alisema FDH itaendelea kushirikiana na TAWA katika kuhamasisha jamii
katika utunzaji wa mazingira na kulinda vivutio vya utalii.
0 Maoni