Wakala ya Barabara za
Vijijini na Mijini (TARURA) imetoa mafunzo
elekezi ya kuwajengea uwezo watumishi wapya 98 wa kada ya Uhandisi, Fundi Sanifu, Maofisa Hesabu,
Wachumi pamoja na Ununuzi na Ugavi.
Mafunzo hayo yamefanyika
katika ukumbi wa Jiji-Mtumba katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.
Mafunzo hayo yaliongozwa
na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bi. Azimina Mbilinyi akishirikiana na Idara
nyingine TARURA Makao Makuu.
Pamoja na hayo watumishi
hao wapya walitakiwa kufanya kazi kwa weledi na ufanisi na kufuata maadili ya
utumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Katika mafunzo hayo watumishi hao walipatiwa mada nyingine
kuhusiana na sheria, kanuni na taratibu
za utumishi wa umma pia walikula viapo vya uadilifu wa utumishi wa umma kutoka
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
0 Maoni