Rais wa Marekani, Donald
Trump, amesema kuwa kampuni ya Coca-Cola imekubali kutumia sukari halisi ya
miwa katika vinywaji vyake vinavyouzwa Marekani.
Kwa sasa, Coca-Cola
hutumia shira ya mahindi katika bidhaa zake za Marekani, lakini Waziri wa Afya,
Robert F. Kennedy Jr., ameeleza wasiwasi wake kuhusu athari za kiafya za
kiambato hicho.
"Nimekuwa
nikizungumza na Coca-Cola kuhusu kutumia sukari halisi ya miwa katika Coke
inayouzwa Marekani, na wamekubali kufanya hivyo," Trump ameandika kwenye
mitandao ya kijamii. "Ningependa kuwashukuru wote walioko madarakani ndani
ya Coca-Cola."
Ingawa Coca-Cola
haikuthibitisha wazi mabadiliko hayo ya mapishi, Msemaji wa Kampuni hiyo
alisema wanathamini "hamu na shauku ya Rais Trump" na kuongeza kuwa
"maelezo zaidi kuhusu bidhaa mpya na bunifu katika safu yetu ya Coca-Cola
yatatangazwa hivi karibuni."
Katika chapisho lake la
Jumatano kwenye Truth Social, Trump alisema: "Hii itakuwa hatua nzuri sana
kwao , utaona. Ni bora zaidi tu!"
Wakati Coke inayouzwa
Marekani huwa inatumia utamu wa shira ya mahindi, Coke kutoka nchi nyingine
kama vile Mexico, Uingereza na Australia mara nyingi hutumia sukari ya miwa.
0 Maoni