Mhe. Majaliwa kumuwakilisha Rais Samia Maonesho ya Osaka Japan

 

Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameondoka jana nchini kwenda Japan kumwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maonesho ya World Expo 2025 Osaka.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema pamoja na mambo mengine Mhe. Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahususha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.

Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.

Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajiwa kumalizika Oktoba 13, 2025. Hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho hayo ya kimataifa ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).



Chapisha Maoni

0 Maoni