Tanzania imeendelea kuvutia watazamaji wengi wa kimataifa
katika maonesho ya Expo 2025 yaliyoanza tarehe 13 aprili, 2025 katika Jiji la
Osaka nchini Japan.
Katika maonesho hayo Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya
Utalii Tanzania Bwana Ernest Mwamwaja amesema kuwa tangu wiki ya utalii
iliponza banda la Tanzania limekuwa limekuwa kivutio na kupokea wageni wengi
wanaotembelea na kutaka kujua fursa vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji
kwenye maeneo ya utalii yaliyopo Tanzania.
Bwana Mwamwaja amesema kuwa Tanzania itatumia maonesho hayo
makubwa duniani pamoja na kupokea watembeleaji na kuwapa maelezo kuhusu fursa
zilizopo Tanzania na kushiriki mijadala ya kimkakati yenye lengo la kuvutia
wageni kutembelea Tanzania.
Amesema kuwa Tanzania imekuwa ikitumia fursa ya Maonesho
hayo ya kimataifa kuelezea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo kama mbuga
za Wanyama zikiwepo Ngorongoro, Serengeti,Manyara, Mikumi, Mlima Kilimanjaro na
maeneo ya fukwe ikiwemo zilizopo
Zanzibar.
Kwa upande wake Afisa Utalii Mkuu,masoko kutoka Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro Bwana Michael Makombe amesema watembeleaji wengi katika
maonesho hayo wamekuwa wakijifunza kuhusu namna Tanzania ilivyofanikiwa
kuimarisha uhifadhi wa wanyama pori.
Maonesho ya mwaka huu yanakadiriwa kutembelewa na watazamaji zaidi ya milioni 26 yakihusisha waoneshaji kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Na. Hamis Dambaya, Osaka-Japan

0 Maoni