Mkurugenzi wa Uchaguzi
Ramadhani Kailima amesema vyama vya siasa 18 vya vimeridhia kusaini Kanuni za
Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2025 na hivyo kupata
sifa ya kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu sambamba na
chaguzi nyingine zote ndogo zitakazofanyika ndani ya miaka mitano ijayo.
Akizungumza katika hafla ya
kusaini kanuni za maadili, Kailima ameeleza
wajibu wa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi kwa mujibu wa kifungu
namba 162(2) cha sheria hiyo pamoja na aya ya 1.2 ya kanuni za maadii ya
uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2025, kanuni zinapaswa kusainiwa na wahusika kwa kila
chama cha siasa, serikali na Tume.
Kailima amevitaja vyama
hivyo vilivyotia saini Kanuni za Maadili ya Uchanguzi Mkuu 2025 kuwa ni chama
cha AAFP, ACT WAZALENDO, ADA-TADEA, ADC, CCK, CCM, CHAUMA, CUF, MAKINI, DP,
NCCR-Mageuzi, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD na UPDP.
Ameeleza kwamba chama kimoja
tu cha siasa ambacho hakijatia saini Kanuni za Maadili ya Uchanguzi Mkuu 2025
ambacho amekitaja kuwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kati ya
vyama 19 vilivyosajiliwa.
Kailima amesema chama
ambacho hakijasaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi leo hakitaruhisiwa kushiriki
uchaguzi mkuu wa mwaka huu na chaguzi zote zitakazitokea katika kipindi cha
miaka mitano ikiwemo uchaguzi mdogo.
0 Maoni