Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto
Biteko ameshiriki katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapimduzi
Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika Viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba,
Zanzibar.
Mgeni wa Heshima katika Sherehe hizo alikuwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Viongozi wengine wa Kitaifa waliohudhuria Sherehe hizo ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu
wa Rais, Mhe. Dkt. Phillip Mpango, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.
Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Viongozi wengine Wastaafu wa
Serikali zote mbili.





0 Maoni