Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu,
amesema maneno ya baadhi ya watu wanaomshambulia mitandaoni hayamuogopeshi asiendele
na majukumu yake ya kisiasa.
“Maneno yao
hayaniogopeshi, mimi natembea na risasi mgongoni hivyo siwezi kutishwa na
maneno ya mashujaa wa mitandaoni,” alisema Lissu.
Lissu
alikuwa akijibu maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari leo Desemba 10, 2024,
Jijini Dare s Salaam kuhusiana na mashambulizi ya maneno mitandaoni yanayofanywa dhidi
yake.
“Mimi natembea na risasi mgongoni, nitaogopa
mawe ya mitandaoni ?, natembea na risasi ipo hapa mgongoni nitaogopa nanii?, Niliitwa
mhaini na wakatumwa watu mnafahamu yaliyoendelea, sasa nitaogopa hawa mashujaa
wa mitandaoni,” alihoji Lissu.

0 Maoni