Mamlaka ya
Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imezindua msimu wa kampeni ya kuhamasisha
utalii kwa wananchi kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka yenye kauli
mbiu isemayo MERRY AND WILD, NGORONGORO AWAITS
ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 4 Desemba, 2024 hadi tarehe 4 Januari,
2025.
Akitangaza
kampeni hiyo Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Idara ya
huduma za utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa katika utekelezaji wa
kampeni hiyo NCAA itashirikiana na kampuni ya Smile Safaris ya Jijini Arusha
ambayo katika kuratibu safari hiyo imeandaa vifurushi (Packages) katika makundi
matatu ili kuwawezesha watanzania wengi
kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro.
Kamishna
Kobelo ameeleza kuwa kifurushi cha kwanza kinaitwa FARU ambapo gharama yake kwa
mtu ni Shilingi 450,000, watakaolipia gharama hiyo watafanya utalii kwa siku
mbili (02) hifadhi ya Ngorongoro na gharama hizo zitajumuisha kiingilio,
Malazi, Chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha ambapo
watakaolipia kifurushi hicho safari ya Ngorongoro itafanyika tarehe 24-25
Desembaa 2024.
Kifurushi
cha Pili kinaitwa TEMBO chenye gharama ya Shilingi 130,000 kwa mtu, kifurushi
hiki kinahusisha utalii kwa siku moja (01) Day trip Ngorongoro na gharama hizo
zitajumuisha kiingilio, Chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha.
Kifurushi
cha tatu kinaitwa CHUI chenye gharama ya Shilingi 85,000 kwa mtu na gharama
hiyo itajumuisha Usafiri wa basi, kiingilio, Chakula, muongoza watalii na
huduma ya picha.
Katika
utekelezaji wa Kampeni hiyo NCAA inatumia vikundi mbalimbali vya Sanaa
vikiongozwa na vijana wa Action Rollers Skates na Makachu Jumpers ambao
watakuwa katika mitaa mbalimbali kwenye
mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar kuanzia tarehe 4 hadi 16 Desemba,
2024.
Katika
utekelezaji wa kampeni ya kuhamasisha utalii, wananchi wote wanakaribishwa
kutembelea vivutio vilivyoko katika eneo laa hifadhi ya Ngorongoro na wanaweza
kuchagua kifurushi chochote kati ya vitatu vilivyotangazwa kwa kupiga namba za
simu 0755 559013 ili kuweka nafasi (booking).
0 Maoni