Kutokea changamoto za mfumo wa usajili BRELA

 

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inautaarifu umma na wadau wake kuwa inatarajia kufanya maboresho ya miundombinu ya mfumo wake wa usajili kwa njia ya mtandao (ORS), kwa muda wa siku mbili.

Taarifa iliyotolewa na BRELA imesema matengenezo hayo yanafanyika kuanzia leo Desemba 20, 2024 majira ya saa 12:00 jioni hadi tarehe 23 Desemba 2024 saa 1:30 asubuhi. Wakati wa maboresho hayo baadhi ya nyakati za kukatika kwa mfumo zinaweza kutokea.

BRELA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaoweza kujitokeza kutokana na maboresho hayo, imemalizia taarifa hiyo.



Chapisha Maoni

0 Maoni