Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa
Dodoma, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Ndugu Charles Saimon Mamba, wametembelea
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa lengo la kujifunza na kujionea vivutio vya
wanyamapori na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa.
Katika ziara hiyo walioifanya jana, kamati ilipata fursa
ya kushuhudia wanyamapori mbalimbali kama vile tembo, simba, twiga, na
pundamilia.
Aidha walitembelea miradi ya kimkakati inayolenga
kuboresha huduma za utalii, ambayo imetekelezwa kwa fedha zilizotolewa na
serikali kwa ajili ya kukuza utalii wa ndani na kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo alisifu juhudi za serikali na
TANAPA katika kuboresha miundombinu na kuhifadhi maliasili, akiwahimiza
Watanzania kuendelea kuthamini na kutembelea hifadhi za taifa.



0 Maoni