Mbunge wa
Same Magharibi, Mhe. David Mathayo, amerejea kwa wananchi wake kutekeleza ahadi
kwa kutoa mifuko 100 ya saruji ya kujenga nyumba ya mwalimu katika shule ya
msingi Nasuru, shilingi 1,760,000 kwa ajili ya madirisha ya nyumba ya mwalimu
pamoja na mabati hamsini ya nyumba hiyo.
Pia, Mhe.
Mathayo amekabidhi shilingi 2,000,000 kwa ajili ya milango ya nyumba hiyo ya
mwalimu, shilingi 350,000 kwa ajili ya kununua kipimo cha Zahanati, shilingi
400,000 kwa ajili ya pumpu ya kumwagilia bustani ya mbogamboga ya kikundi cha
vijana.
Kama hiyo
haitoshi, Mhe. Mathayo ameahidi kuwasomesha vijana wanaotaka kusomea cheti cha
udereva wa malori ili waweze kupatiwa leseni ya udereva wa malori, na kuwaahidi
kwamba watakapo faulu na kupata leseni atawaajiri kwenye kampuni yake.
“Kesho
asubuhi mmoja wenu au kiongozi wenu mtakayemchagua aje mimi nitawapatia
shilingi laki nne kila mmoja ili mkasomee mje niwajiri kwenye kampuni yangu,
kwa sababu mimi nataka vijana waaminifu, nawapo niliowachukua kutoka hapa
Nabangalala wako huko nafanyanao kazi,” alisema Mhe. Mathayo.
Kwa upande
wao vijana hao wamemshukuru mbunge wao huyo kwa kuwawezesha kwenda kupata elimu
itakayowasaidia kuweza kupata leseni ya kundesha malori kwa kuwa kilichokuwa
kinawakwamisha ni fedha za kusomea cheti licha yao wao kujua kuendesha malori.
Baadhi ya
wananchi waliohudhuria kikao cha mbunge huyo wamempongeza kwa kutimiza ahadi
mbalimbali anazotoa na kusaidia kuboresha shughuli za maendeleo na kiuchumi za
wapiga kura wake wa jimbo la Same Magharibi.



0 Maoni