Wanakijiji
wa Kijiji cha Nyasaungu wameanza kuwa na matumaini ya kupata huduma ya
matibabu katika Zahanati yao ifikapo Desemba mwaka huu, baada ya ujenzi wake
kukamilika.
Taarifa
iliyotolewa na Mbunge wa Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo imesema kijiji
hicho chenye vitongoji vitano kwa sasa kinakamilisha ujenzi wa Zahanati yake.
Kijiji hiki
ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu, vijiji vingine ni Kabegi na
Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake, imeeleza taarifa hiyo.
“Kwa hiyo,
ifikapo Desemba 2024, kila kijiji ndani ya Kata ya Ifulifu kitakuwa na zahanati
yake, hatua kubwa sana ya maendeleo kwenye Kata hii,” Imesema taarifa ya Prof.
Muhongo.
Taarifa hiyo
imeeleza vyazo vya fedha vya Zahanati ya Nyasaungu kuwa ni michango ya
wanakijini na mbunge wa Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo.
Katika
kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo Prof. Muhongo alipiga Harambee mbili za kupata
fedha za kuanza ujenzi wa zahanati hiyo. Wanakijiji wanachangia nguvukazi.
Pamoja na
vyanzo hivyo, pia Serikali Kuu imechangia jumla ya shilingi milioni 100.

0 Maoni